Translate

Tuesday, January 10, 2023

AJIRA YA MTANZANIA

 

NJIA 6 HALALI ZA KUJIAJILI MWENYEWE
Mara nyingi nimesikia watu wengi wakiulizia michongo ili wapate sehemu ya kupata pesa. Kiuhalisia ukiulizia mchongo hapa tayari ushakuwa tayari kuajiliwa, sio vibaya kuajiliwa inategeamea umeajiliwa wapi na kipato unachopata kama kitakulidhisha japokuwa kwa kijana wa siku hizi sikushauri sana kualijiwa kwani hasara nyingi unazipata ukiwa kwenye ajira. Angalia hapa madhara ya kuajiliwa.


Tuachanena hayo turudi kwenye maada yetu, Je ni wapi unaweza kujiajili na ukajitegemea kiuchumi kwa 100%.  Nikiwa darasa la nne, mtunzi mmoja alitunga shairi moja akisema "NIKIMALIZA KUSOMA NITAFANYA KAZI GANI" lakini hapao hapo labla ya kutoka darasana hilo hilo nikakutana na mtunzi mwingine katatua tatizo kwa kuonesha njia ya kupata Mali kwa shairi lake la KAMA MNATAKA MALI MTAIPATA SHAMBANI. Maana yangu ni ipi? Kiukweli katika moja ya maswali yanayosumbua vichwa vya vijana wengi hasa wanaomaliza masoma yao ni kupata kazi ya kufanya ili waweze kuingiza kipato.

Je, ni kweli wote tuingie shambani?

Jibu ni hapana, kwani tukienda shambani wote tutapata nani atatuuzia nguo tuvae, nani atatuletea sabni viberiti, chumvi nk kwa matumizi ya ndani? Nani atatusafirishia bidhaa zetu kutoka aidha shambani au kwenda sokoni? na Nani atatusajilia laini kwa ajili ya kupata mawasiliano? Hapa ni kwamba shambani wataenda baadhi na wengine wataenda maeneo mengine tofauti. Zipo njia zaidi ya 1000 ambazo binadamu wanazitumia kujipatia kipato na kuweza kuendesha maisha yao kila siku huku ikuonekana kuwa watu waliojiajili ni wengi kuliko walioajiliwa. Sikatazi watu wasiajiliwe ila nataka mtu ambaye amekosa ajila afaidike ikiwezekana zaidi ya aliyeajiliwa. Ndiyo inawezekana kabisa. Chamsingi soma makala zangu zote ili kujua mengi zadi. Makala hii ina link nyingi sana ila neno la blue ukiligusa linakupeleka sehemu husika ili kukusaidia pale ambapo hujaelewa, kwa maana ya kwa Kuna makala nyingine nilikuea nimezichapisha na siwezi kuzirudia kama zilivyo, nakuelezea kisha nakupeka sehemu husika.

Kwa nini nikushauri kujiajili hali upande mwingine unaona huna mtaji wowote?.

Ukweli ni kwamba watu wengi waliojikomboa kiuchumi asilimia kubwa hawajaajiliwa bali wameajili watu kuwatumikia huku wao wakiendelea kupata burudani, watoto wao wakisoma shule nzuri ikiwa waajiliwa bado wanahangaika na maisha. Kuna dhana potofu kwamba kujiajili Hadi uwe mtaji ndipo uanze, lakini jiulize mtaji huo unaupata wapi?  Ndio maana nimekuletea njia hizi kuu nane ambazo kila siku tunakutana nazo na zipo karibia maeneo yote ya nchi hii.
Hapa utajifunza namna ya kuanza kujitegemea ukiwa kijana.
Hizi hapa ni njia kuu sita za kupata kipato halali ambako unaweza ukajiajili mwenyewe.

1. Anzisha biashara.
Biashara ni sekta ambayo inakua haraka na inaweza kukuwezesha kupata kipato ambacho unaweza kuendesha maisha yako na familia yako. Mfano, katika ripoti ya mwaka 2019 inaonesha asilimia 66.3  ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wanaishi kwa kutegemea bishara, hiki ni kiwango kikubwa sana na uaweza kuona ni kwa jinsi gani watu wanaweza kutoboa kupitia biashara Unaweza kuanzisha biashara bila mtaji wowote au ukiwa na mtaji wako ndipo utapata faida nzuri.
Je ni biashara gani ufanye ili kukupatia kipato kikubwa? 
Zipo biashara nyingi sana ambazo kiuhalisia zimeshikilia maisha ya watu wengi, Kuna baadhi ya biashara ambazo unazidharau lakini Kuna watu zinawaigizia zaidi ya laki kila siku. Soma hapa biashara na miradi 154 ambazo inaweza kuanzisha. Ushauri ni kwamba usiwe na tamaa eti kila biashara ufanye, angalia wazo ambalo wewe unalipenda na uanze kufuatilia kwa undani zaidi, Nasisitiza kuwatumia wenyeji wa biashara husika ili kuijua kiundani zaidi. Pia sikushauri usikilize mawazo ya mtu mmoja nikushauri kusikiliza mawazo ya watu angalau watatu na ujenge hoja yako ambayo itakuwa imara Kisha anza

2. Kuwa wakala
Uwakala sasa umekuwa katika mada pana zadi kwani sasa kuna zaidi ya aina 100 za mawakala, Unaweza kuwa wakala wa kampuni mfano CRDB, Vodacom n.k au wakala wa kutuma na kupokea bidha aidha mjini au vijijini au hata bidhaa za mtandaoni. Hii ni sekta ambayo inafaida kubwa sana hata kama huna mtaji kabisa. Nikuachie changamoto "fikiria ni kitu gani ambacho unaweza kusimamia au kutekeleza ambacho kiuhalisia wewe sio mmiliki.
Utofauti kati ya wakala na mwajiliwa ni kwamba hata kama wote wanafanya kampuni moja ni kwamba mwajiliwa mshara wake umepangwa na haubadiliki, wakala anapata pesa kutokana na juhudi zake haina kiwango kikubwa wala kidogo ni juhudi tu.
Je, umeshawahi kufikiria kuwa wakala wa kusajili laini mtaani anweza kuingiza hadi milioni au zaidi kwa mwezi?. Soma makala hizi kwa ajili yako. 
Jinsi ya kuwa wakala wa kusajili laini na jinsi unavyopata pesa.


Jinsi ya kuwa wakala wa kutuma na kupokea pesa M pesa Tigo pesa n.k na mabenki kama NMB, CRDB n.k


Pia unaweza kuwa wakala wa kusambaza bidha aidha za watu binafsi, makampuni au mtandaoni. Kwa bidhaa za watu binafsi hakuna ugumu sana lakini kwa bishara za makampuni unakubidi uwe na muda wa kutosha na kwa upande wa bishara za mtandaoni ni uwezo wako wa kutangaza bidhaa hizo na wewe ndipo unapata pesa nzuri.
Jifunze njia za kutangaza biashara mtandaoni.

3. Anzisha kilimo.
Kilimo ni sekta mabayo imeajili asilimia 62 ya watanzania wote. Kilimo ndiyo kazi ambayo unawezakufanya hata kama huna pesa kabisa ili hali una nguvu za kufanya kazi. Kilimo ni sekta kubwa sana iliyosheheni mazao mbalimbali ambayo unaweza kuanza kulima hadi sasa hivi na ukaanza kupiga pesa.

Unawezaje kufanikiwa katika kilimo?

Kuna njia nyingi sana ila mimi nimekuandalia hizi hapa kukupa mwanga

_Anzisha kilimo ambacho watu wengi hawalimi katika maeneo uliyopo na yanauhitaji.
_Lenga kuvuna mazao yako katika msimu wa uhaba wa zao hilo.    

 _Jikite sana katika kilimo cha imwagilaji kwani wengi hawafanyi hivyo na faida yake inakuja haraka
Namna ya kujua zao linalolipa katika mazingiza uliyopo.
*Tafuta zao ambalo lina uhitaji mkubwa na upatikani wake mdogo
*Kama no mgeni katika mazingira fulani, *watumie wenyeji kupata taatifa za mazao yaliyopo.
*Kama ikibidi tafuta watu wa kukusadia kupata mawazo.
*Watafute watalaam ili kujua mahitaji ya zao hilo na sehemu ambayo unaweza kuvuna kwa asilimia mia moja.


Mambo ya kuepuka
_Epuka kutelekaza shamba bila uangalizi wa karibu
_Epuka kuamini sana wafanyakazi fika shamabani mara kwa mara ikiwezekana
_Epuka kulima kwa kufuata mkumbo, hapa hakuna cha wengi wape.
_Epuka kushikiana na mtu kwa kushawishi sana, shirikiana na wenye nia tu itakupunguzia migogoro na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shamba
_Epuka kuwekeza katika mazingira yasiyoaminika.

4. Anza ufugaji.
Hapa ndipo pesa ilipojificha kwa sasa, mfano mdogo tu, yai moja linauzwa hadi shingi mia tano wakati mahindi kilo inaweza kushuka hadi mia tatu maeneo ya vijiji hapo ndipo ulinhanishe thamani ya vitu hivyo kwa sasa. 
Takwimu zinaonesha watu wenye utapiamlo katika nchi zianzoendelea ni takribani watu milioni 827 hivyo kulingana na takwimu hizi bado kuna uhitaji mkubwa wa protein hasa kutoka kwa wanyama Kama kuku, sungura n.k
Unaweza kufuga mfugo wowote uupendao kama aidha kuku, bata, mbuzi, ng'ombe, nguruwe  n.k 
Kama kilimo na ufugaji ni sehemu kubwa siwezi kuelezea kwa upana zaidi hapa hatutamaliza, ila nimekuandalia vitini mbalimbali vya maelekezo jinsi ya kufunga kitaalamu kwa kila mfugo ili kukupa mwanga ili uweze kuanza. 

5. Ingiza pesa kupitia mtandao.

Hapa watu wengi wanaingiza mamilioni ya pesa kila mwezi. Kama wewe ni mtu wa mtandaoni hapa ni sehemu yako. Unaweza kuapata pesa kupitia Google AdSense ambayo ndiyo kampuni kubwa na ya kuaminika kwa watu wa YouTube na blog/website. Kama blog yako ni ya kiswahili au unaweka content za wakubwa unweza kutumia Propellarads au Adsterra na ukaendelea kupata pesa. Pia  Facebook, Instagram, WhatsApp n.k zinaweza kukupatia pesa kubwa kwa kutangaza bidhaa na kushare link
Tahadhali ni kwamba usitake kufanya kazi mtandaoni ukihisi ni kazi nyepesi, ni kazi ngumu sana hasa mwanzoni na wengi wanakata tamaa. Itakuhitaji kuchukua muda wako kila siku na bando na utaumuza kichwa ili kupata pesa. 
Tahadhali nyingine usitake kupata pesa kilahisi kwenye site au app zinazotoa pesa mtandaoni bila kufanya kazi maana hiyo pesa mara nyingi haitoki au haifiki kiwango cha kutoa. 
Nikushauri kuchagua kwenye kampuni za matangazo Kama AdSense, AdMob na Facebook audience kwa application, ama za bidhaa kama amazoni.

Pia ifahamu Google AdSense kwa undani zaidi.

Kama una swali lolote usisite kuuliza kwenye sehemu ya comment hapo chini.

Jisajili kwa email kisha  na ithibitishe kisha uliza swali lolote nitakujibu na nisipokujibu mimi wanafamilia wa fungua mbongo watakujibu.

6.Jiajili kufanya kazi mtandaoni ukiwa nyumbani.
Fivver ni mtandao mkubwa unatoa fursa ya kufanya kazi, kama unajuzi wowote wa mtandao kama photo editing, typing, web design, logo design, YouTube channel creation  n.k hii ni sehemu yako nzuri.

AJIRA YA MTANZANIA

  NJIA 6 HALALI ZA KUJIAJILI MWENYEWE Mara nyingi nimesikia watu wengi wakiulizia michongo ili wapate sehemu ya kupata pesa. Kiuhalisia ukiu...